The House of Favourite Newspapers

Mbeya: Polisi Wafukua Jeneza la Aliyekufa na Kuzikwa, Baadaye Mwili Wake Kukutwa Kitandani

mbeya-1

MBEYA: WAKAZI wa eneo la Isanga katika Jiji la Mbeya wameendelea kushuhudia visa, mikasa na matukio ya vioja, baada ya mtoto HARUN JAILO KYANDO mwenye umri wa miaka 9 alikufa na mwili wake kuzikwa jana kwenye makaburi ya Isanga jijini humo ambapo baadaye  mwili wake ulikutwa kitandani nyumbani kwao mara baada ya waombolezaji kurejea kutoka makaburini.

mbeya-2

Wananchi wakiwa wamejaa makaburini kushuhudia tukio la kufukua jeneza hilo.

Waombolezaji waliporudi nyumbani walitaharuki kuona mwili wa marehemu mtoto HARUN JAILO KYANDO ukiwa chumbani umelazwa eneo ulipokuwa awali.
Kutokana na hali hiyo taarifa zilifikishwa Polisi mara moja, askari Polisi walifika na kurejesha hali ya amani kwa kuuchukua mwili wa marehemu ambao kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

mbeya-4

Jeneza mara baada ya kufukuliwa.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limesimamia zoezi zima la kufukua jeneza hilo na baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo, kilichokutwa ni jeneza tupu likiwa halina kitu chochote.

Kwa pamoja wananchi na wanafamilia walikubaliana asubuhiya leo kwenda kufukua kaburi hilo ili waone nini kilichozikwa, na hivi dakika hizi zoezi hilo linaendelea na picha za makaburini hapo.

mbeya-3

Taratibu nyingine za mazishi zitafanyika leo tarehe 17.01.2017. Mpaka sasa bado haijafahamika ni uzembe /bahati mbaya wafiwa kusahau kuweka mwili wa marehemu kwenye jeneza au kulikuwa na hujuma zozote.

mbeya-3

Jeneza hilo likibebwa na Jeshi la Polisi.

Mbeya: Maiti Iliyozikwa Yakutwa Kwenye Godoro Chumbani

Comments are closed.