The House of Favourite Newspapers

Polisi Wakamata Silaha, Jambazi Hatari Dar

1-kamishna-wa-polisi-kanda-maalum-dar-es-salaam-cp-simon-sirro-akizungumza-na-wanahabari-hawapo-pichani-001Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam CP, Simon Sirro akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).2-akisikiliza-maswali-yaliyokuwa-yakiulizwa-na-wanahabari-001…Akisikiliza maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari.

3-kamanda-simon-sirro-akionyesha-baadhi-ya-silaha-zilizokamatwa-001Kamanda Simon Sirro akionyesha baadhi ya silaha zilizokamatwa.4-kamanda-sirro-akionyesha-gari-lililokamatwa-na-magunia-ya-bangi-001Kamanda Sirro akionyesha gari lililokamatwa na magunia ya bangi .

6-taswira-ya-mbele-ya-gari-hilo-lililokamatwa-na-magunia-ya-bangi-001Taswira ya mbele ya gari hilo lililokamatwa na magunia ya bangi.

5-wanahabari-wakichukua-tukio-hilo-001Wanahabari wakichukua tukio hilo.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 27.09.2016

  KUPATIKANA KWA SMG 01, MARK IV 01, BASTOLA 01 NA RISASI 12 

  • KUKAMATWA KWA JAMBAZI  HATARI ANAYESHIRIKIANA NA MKEWE KATIKA MATUKIO YA UJAMBAZI WAKUTUMIA SILAHA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar Es salaam kupitia Kikosi Maalum cha Kupambana na Ujambazi wa kutumia silaha kimefanikiwa kumkamata jambazi hatari anayehusika kwa makosa ya ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali Jijini Dar Es Salaam.

Mnamo tarehe 23/09/2016 saa nane na nusu mchana maeneo ya Kimara mwisho Askari walimkamata BAKARI ABDALAH miaka 40, mkazi wa vijibweni  ambaye anajihusisha katika matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha. Katika mahojiano amekiri kushiriki matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha. Aidha aliwaelekeza askari nyumbani kwake alikoficha silaha hiyo, Polisi katika ufuatiliaji walifika nyumbani kwa mtuhumiwa huyo tarehe 26/09/2016 maeneo ya Kigamboni/vijibweni CCM walipofanya upekuzi  wakafanikiwa kupata bastola aina ya BROWNING yenye usajili wa No.CAR A081900 ikiwa na magazine mbili na risasi tano pamoja na simu aina ya Nokia Lumia ambayo iliporwa katika tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha huko maeneo ya Mivumoni mkoa wa kipolisi Kinondoni.

Pia mke wa mtuhumiwa aitwaye sabiha omary miaka 28, anashikiliwa kwa tuhuma za kushirikiana na mume wake katika matukio mbalimbali ya unyang’anyi wa kutumia silaha maeneo mbalimbali jijini Dsm. Watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa watapelekwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika.

Katika tukio lingine mnamo tarehe 26/09/2016  majira  ya saa nne usiku maeneo Viwege kwa Bilali Pugu mkoa wa kipolisi Ilala Askari wakiwa doria na ufuatiliaji wa wahalifu wanaojihusisha na uporaji wa kutumia silaha waliwatilia shaka watu wawili wakiwa kwenye pikipiki ambayo namba zake za usajili zimefutika, walipoona askari wanaelekea usawa wao mmoja aliruka katika pikipiki hiyo na kutupa begi na kukimbia na mwenye pikipiki alitoweka kwa kuendesha pikipiki yake kwa kasi na kuelekea porini. Polisi walipopekua begi hilo walikuta silaha aina ya SMG iliyofutwa namba zake za usajili, ikiwa na magazine na risasi saba ndani yake. Juhudi za kuwasaka watuhumiwa hao zinaendelea ili kubaini matukio waliyowahi kufanya.

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dar es salaam mnamo tarehe 21/09/2016 majira ya saa 11:00 jioni huko Tegeta karibu na shule ya sekondari ya Fedha mtaa wa makumbusho  askari wakiwa doria  waliwatilia mashaka watu watatu wakiwa wamekaa katika kichaka  na walipowaona askari walikimbia na kuacha silaha moja kukimbia na kuacha silaha moja aina  MARK 4 yenye usajili wa TZCAR 86274.

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA 22 WANAOJIITA WANACHAMA WA CUF JIJINI DSM, WAKUTWA NA DHANA ZA KUFANYIA UHALIFU

Mnamo tare 25.09.2016 huko Mwananyamala, Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar Es salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 22 ambao ni Wanachama wa CUF wakiwa na zana za kufanyia uhalifu kama Mapanga, Jambia na Visu 05 pamoja na chupa za kupulizia (spray) zikiwa kwenye boksi zenye chupa 10 zenye maandishi ya Kichina. Watuhumiwa hao walipanda gari la abiria (COSTER) yenye namba ya usajili T.857 CHE  inayopita njia ya BUGURUNI –MWANANYAMALA.

Watuhumiwa hao walikamatwa baada ya askari kupata taarifu kwamba wamekuja Dsm kwa ajili ya kufanya fujo kwenye ofisi hiyo pamoja na kuichoma moto. Walipohojiwa zaidi walieleza kuwa  wao ni wanachama wa chama cha CUF kutoka UNGUJA kutoka kwenye matawi mbalimbali wamekuja kwa ajili ya kazi maalum na wako katika kitengo cha ulinzi na kueleza kuwa wapo zaidi ya watu 100.

Katika mahojiano zaidi wameeleza kuwa wamekuja jijini Dar Es salaam kwa maelekezo ya kiongozi wao wa CUF NASSORO AHAMAD MAZRUI ambaye ni Naibu Katibu mkuu wa CUF ambaye aliwaamuru kuungana na walinzi wenzao  wengine waliopo ofisi za chama chao Makao makuu Buguruni.

Watuhumiwa wote 22 wanaendelea kuhojiwa na majina yao ni kama yafuatayo;

  • SAIDI MOHAMED ZAHARANI, alikamatwa na boksi ya spray
  • HAMISI HAMISI alikamatwa na kisu
  • MOHISINI ALLY alikamatwa na kisu
  • MASOUD IGASA FUMU alikamatwa na kisu
  • JUMA OMARY(6) MBARUKU HAMISI(7) JUMA HAJI MWANGA(8) HAMISI NASSORO HEMEDI(9) MOHAMED OMARY MOHAMED(10) NASSORO MOHAMED ALLY NA WENGINE 12

 POLISIKANDAMAALUM DSM WAKUSANYA TSH 767,790,000/=KUPITIA TOZO ZA MAKOSA YA USALAMA BARABARANI NDANI YA SIKU KUMI

Jeshi la Polisi Kanda maalum Dsm kupitia kikosi chake cha usalama barabarani kimekamata makosa mbalimbali ya usalama barabarani kwa kipindi cha kuanzia tarehe 16.09.2016    hadi tarehe 26.09.2016 na kuingizia serikali mapato ya ndani kama ifuatavyo;

  1. Idadi ya magari yaliyokamatwa         – 22,388
  2. Idadi ya Pikipiki zilizokamatwa         – 3,205 
  3. Daladala zilizokamatwa – 8,344
  4. Magari mengine (binafsi na malori)                     – 14,044
  5. Bodaboda waliofikishwa Mahakamani

kwa makosa ya kutovaa helmet na

kupakia mishkaki                                              –  52

  1. Jumla ya Makosa yaliyokamatwa           – 25,593

Jumla ya Fedha za Tozo zilizopatikana TSH 767,790,000/=

JESHI LA POLISI KUIMARISHA ULINZI WAKATI WA MECHI YA WATANI WAJADI KATI YA SIMBA DHIDI YA YANGA ITAKAYOFANYIKA TAREHE 01/09/2016

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar Es salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama imejipanga ipasavyo kuhakikisha mchezo  kati ya SIMBA dhidi ya YANGA wenye mvuto mkubwa kwa washabiki wa Tanzania, nchi za Afrika mashariki na Afrika nzima kuchezwa katika hali ya usalama.

Aidha tunaomba wananchi wasiwe na shaka yoyote ya kiusalama na pia watupe ushirikiano wa kutoa taarifa kwa jambo lolote watakaloliona kuwa linaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani kwa kipindi chote watakapokuwa nje au ndani ya uwanja. Kutakuwa na CCTV Camera ili kuhakikisha sehemu zote mageti ya kuingilia na kutokea na maeneo yote yanaonekana na kuweka kumbukumbu za matukio yote.

Pamoja na hayo wananchi wanatakiwa kuwa watulivu katika kushangilia mechi hiyo, na kuepuka kufanya mambo yafuatayo:

  • Kuingia na chupa za kimiminika cha aina yeyote,
  • Kuingia na silaha ya aina yoyote
  • Kupaki magari ndani ya uwanja
  • Kukaa sehemu ambazo tiketi zao haziwaruhusu.

 KUKAMATWA KWA GUNIA SABA YA BHANG YENYE KILO 560 HUKO KIMARA

Mnamo tarehe 25/09/2016 majira ya saa sita na nusu mchana maeneo ya  mbezi  njia panda ya mpigi  magohe  askari wa usalama barabarani aliitilia mashaka gari T172 DEQ Toyota Verosa rangi ya silver ikiendeshwa na dereva  aitwaye HASAN ABDALAH BANDA,  miaka 20, mkazi wa msasani mkoa wa Polisi Kinondoni.

Alipomsimamisha kwa lengo la kumhoji dereva alikaidi amri ya kusimama  badala yake aliongeza kasi zaidi,  ndipo askari huyo aliwasiliana na askari mwingine ilikoelekea gari hilo na kufanikiwa kukamatwa mtuhumiwa maeneo ya Mbezi  Kibanda cha mkaa. Mtuhumiwa huyo alipelekwa kituo cha Polisi Kimara. Gari ilipopekuliwa ilikutwa na gunia saba za bhangi ambayo yana jumla ya kilo 560. Mtuhumiwa atapelekwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika.

S.N.SIRRO – CP

 KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM

DAR ES SALAAM.

Comments are closed.