The House of Favourite Newspapers

Polisi: Wapo WaTZ Wahusika Mashambulizi Mpakani na Msumbiji

0

POLISI nchini imesema kwamba kuna raia wa Tanzania wanaohusika na mashambulizi yanayofanyika mpakani mwa Msumbiji na Tanzania.

 

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo katika Jeshi la Polisi Tanzania, Liberatus Sabas, amesema  baadhi ya mashambulizi yanayotokea katika eneo la kusini mwa Tanzania mpakani na Msumbiji yanafanywa na vijana waliotoroka Tanzania baada ya kufanya vitendo kama hivyo katika mikoa ya Pwani na Tanga.

 

Amesema  licha ya matukio hayo ya mashambulizi kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa, jamii ya Watanzania inatakiwa kufuatialia kwa karibu  mienendo ya vijana katika jamii ili kukomesha hali ya vijana kujiunga na makundi ya uhalifu.

 

Amefafanua kwamba baadhi ya vijana hao walitoroka shule na kujiunga na makundi hayo, akaongeza kwamba polisi nchini imewakamata watu kadhaa wakihusishwa na  mashambulizi hayo.

 

Kwa mujibu wake, ukamataji huo unaendelea kwa ushirikiano wa maafisa wa usalama wa Tanzania na Msumbiji.

 

Nyumba kadhaa zimeteketezwa kwa moto, watu kuuawa na kujeruhiwa katika mashambulizi huko Cabo Delgado, Msumbiji.

Leave A Reply