The House of Favourite Newspapers

Polisi Yafafanua Kamata Kamata ya ‘Vimini’ Dar

JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeeleza kuwa suala la kamata kamata ya watu waliovaa mavazi ambayo ni kinyume na maadili haliko chini ya jeshi hilo na badala yake wao husimamia sheria na kulinda maisha ya watu na mali.

“Suala la mavazi si la Jeshi la polisi. Ukitaka mimi nitoe ufafanuzi wa mavazi, uniulize habari zinzohusiana na unifomu za polisi. hizo niko vizuri,” amesema Kamanda Mambosasa.

 

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipozungumza kwenye kipindi cha ‘Morning Tumpet’ kinachorushwa na runinga ya Azam Two na kueleza kuwa zipo taasisi na mamlaka nyingine zinazohusika na suala la usimamizi wa maadili, utamadunu pamoja na mavazi.

 

Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa Dhima ya Jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa watu pamoja na mali zao na pia kusimamisa sheria zilizowekwa.

“Dhima ya Jeshi la Polisi ni kusimamia sheria, kulinda maisha ya watu na mali. Suala la mavazi, zipo taasisi nyingine,” amesema Kamanda Mambosasa.

 

Jambo hili lilizua taharuki kubwa, baada ya kuchapishwa habari inayoeleza kuwa watu waliovaa vimini na kunyoa viduku wamekamatwa na Polisi. Kichwa cha habari hiyo kiliandika.

Hata hivyo, Kamanda Mambosasa, jana jumatano Januari 17, 2018 akiongea na waandishi wa habari, alikanusha habari hizo na kueleza kuwa ni za uzushi, huku akiutaka uongozi wa gazeti la Nipashe kuomba radhi kwa usumbufu liliousababisha.

Comments are closed.