The House of Favourite Newspapers
gunners X

Polisi Yapiga Mabomu Chadema Waliomfuata Mbowe Segerea

0

POLISI wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliofika gereza la Segerea leo jijini Dar es Salaam kumchukua Mwenyekiti wao,  Freeman Mbowe,  baada ya kumaliza kulipa faini ya Sh. milioni 70 aliyohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwanzoni mwa wiki hii.

 

Miongoni mwa viongozi na wanachama wa Chadema waliofika Segerea ni Mbunge wa Kawe, Halima Mdee. 

 

Mpaka sasa, miongoni mwa viongozi wengine wa chama hicho, wakiwemo Katibu Mkuu, John Mnyika; Naibu Katibu Mkuu, Salum Mwalimu na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche wametoka gerezani baada ya kulipa faini iliyotakiwa na mahakama.

Leave A Reply