The House of Favourite Newspapers

POWER ON FITNESS GYM YAUKARIBISHA MWAKA 2018 KWA MBWEMBWE

Washiriki katika hafla hiyo wakiwa katika staili mbalimbali ya mazoezi ya viungo.
Washiriki wakiwa katika mazoezi ya viungo katika Viwanja Vya Sayansi Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Wakiendelea na mazoezi.
Washiriki wakiwa katika zoezi ya kukimbia (Jogging) kutoka katika viwanja vya Sayansi Kijitonyama kuelekea maeneo ya Mlimani City kupitia makaburi ya sinza kurudi hadi sayansi.
Mazoezi ya kukimbia (Jogging) yakiendelea.
Full kujiachia kwa mazoezi ya Jogging kwa washiriki.
Hafla hiyo ikiendelea.

 

Power on Fitness Gym iliyopo Mwenge, Kinondoni jijini Dar es Salaam imeukaribisha mwaka 2018 kwa staili ya kipekee ambapo wadau mbalimbali wamejumuika kufanya mazoezi pamoja na kuburudika kwa chakula, vinywaji na muziki kabambe wa Skylight Band.

 

Shughuli hiyo imefanyika mapema leo Jumamosi, Januari 27,2018  katika Viwanja vya Posta vilivyopo Sayansi,  Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo shughuli hiyo inatarajia kumalizika usiku mnene.

 

Hafla hiyo imepambwa na mazoezi ya kukimbia (Jogging) ambayo yameanza alfajiri ya saa 12, na kufuatiwa na mazoezi ya Aerobics, steps, zumba, mpira wa miguu, na michezo mingine kama kuvuta kamba na kukimbiza kuku.

 

Baada ya mazoezi kukamilika wadau wa Power on Fitness Gym wamejumuika katika burudani kabambe ya muziki iliyoporomoshwa na bendi ya Skylight na Ma DJ wakali wa hapa nchini.

 

Mbali na burudani hizo kulikuwa na Nyama choma iliyoandaliwa kiufundi na wapishi waliobobea, Supu bila kusahau vinywaji vya kila aina.

 

Shughuli hiyo imedhaminiwa na Kampuni ya JSP Marketing Link Limited ikishirikiana na Msouth Company, Dagaa Microfinance Limited, Simba Makini Group, Jaina Ice Cubes, Micgen Insurance Brokers, TTCL na wenyeji Power on Fitness Gym.

Comments are closed.