The House of Favourite Newspapers

Pretty Kind Alia Maisha Magumu

BAADA ya kufungiwa kufanya sanaa kwa miezi sita na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kutokana na kupiga picha za nusu utupu, msanii wa filamu, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ ameibuka na kulia maisha magumu kwa kuwa hana kazi yoyote anayoifanya.

 

Akizungumza na Za Motomoto News, Pretty Kind alisema kwa sasa maisha yake yamemwendea kombo na amekuwa ombaomba kwa ndugu, jamaa na marafiki kwani alikuwa akitegemea sanaa kwa kila kitu sasa suala la kufungiwa limeharibu kila kitu.

 

“Kiukweli nimenyooka licha ya kwamba ni siku chache tu nimeshakaa bado nyingi zaidi lakini maisha yamekuwa magumu mno naishi kwa kusaidiwa na ndugu kwani kibaya zaidi kabla sijafungiwa fedha zangu zote nilizitengenezea filamu na video ambapo nilibaki sina kitu na hivi niko tu nabahatisha maisha maana niliitegemea sanaa kwa kila kitu,” alisema Pretty Kind.

Na Mwandishi Wetu

Comments are closed.