visa

Prodyuza kutoka Norway atinga Global TV Online leo

Carl Hovind  (1)
Carl Hovind  (4)

Prodyuza Carl Hovind akiwa katika pozi ndani ya studio za Global TV Online.

Na Hashim Aziz- GPL

Prodyuza mahiri, Carl Hovind aliyewahi kufanya kazi na wasanii wakubwa kama Damian Marley, Christopher Martin, Gyptian na Roberto (Amarula) ametua nchini Tanzania na leo ametembelea kwenye studio za Global TV Online zilizopo kwenye ofisi za kampuni ya Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar es Salaam.

Carl Hovind  (2)

Katika mahojiano maalum na waandishi wetu, Carl amesema lengo la safari yake kutoka Oslo, Norway yaliko makazi yake mpaka Dar es Salaam, ni kuja kutafuta vipaji vya wasanii watakaoutangaza muziki wa Tanzania kimataifa.

Prodyuza huyo, ameuambia mtandao huu kwamba tayari ameshaanza kukutana na wasanii mbalimbali wa Kibongo, wakiwemo Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Shaa, Amini  na wengine wengi kwa lengo la kubadilishana mawazo na kuwapa mbinu za kutoboa kimataifa.

Carl Hovind  (3)

“Lengo langu siyo wasanii wakubwa tu, hata wale ambao hawajawahi kuingia studio lakini wana vipaji, nipo tayari kufanya nao kazi. Nitahakikisha Tanzania inakuwa na msanii anayefahamika dunia nzima kwa ubora wa kazi zake,” alisema Carl ambaye atakuwepo nchini mpaka Machi, mwaka huu.
Toa comment