The House of Favourite Newspapers

PROF. NDALICHAKO AZINDUA VIKARAGOSI KWA MASOMO YA DARASA LA 1 NA II

Waziri  wa Elimu, Sayansi na Teknlolojia, Prof. Joyce Ndalichako akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo naye akizungumza jambo.
Mwenyekiti wa Taaisi ya  Elimu Tanzania (TET) akizungumza.
Mmoja wa wadau wa elimu akizungumza jambo kuhusina na jinsi elimu hapa nchini inavyopaswa kupewa kipaumbele.
Prof. Ndalichako akionesha CD yake aliyopewa ya Vikaragosi katika hafla hiyo.
Meza kuu ilivyoonekana.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki uzinduzi huo wa vikaragosi.
Baadhi ya wadau wa elimu wakifuatilia kilichokuwa kikiendelea.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknlolojia, Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.

 

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknlolojia, Prof. Joyce Ndalichako amezindua mfumo wa masomo ya kielektroniki kwa wanafunzi wa darasa la kwanza na la pili kujifunza kwa njia ya Vikaragosi utakaowawezesha wanafunzi hao kujifunza kwa kutumia mifumo ya (Cartoon).

 

 

Prof. Ndalichako akizungumza katika hafla hiyo amepongeza Taasisi  ya Elimu Tanzania (TET) na kueleza kuwa mfumo huo utawawezesha wanafunzi hao kuelewa masomo yao kwa ufanisi zaidi.

 

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Bernadeta Killian ameeleza kuwa uzinduzi huo ni wa awamu ya kwanza ukiwa na lengo la kuboresha ufundishaji na stadi za kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu.

Uzinduzi wa mfumumo huo wa kujifunza kwa kutumia vikaragosi utaongeza wigo na ari ya wanafunzi kupenda masomo yao huku ikiwa ni njia rahisi ya kuongeza maarifa kwa wanafunzi wa darsa la kwanza na la pili hapa nchini.

 

Comments are closed.