The House of Favourite Newspapers

Prof. Tibaijuka Aaga Rasmi Bungeni

0

MBUNGE wa Muleba Kusini, Balozi Profesa Anna Tibaijuka, jana Aprili 3, 2020, amewaaga rasmi Wabunge wenzake na kusema Bunge lijalo atakua ameng’atuka madarakani na kwamba anaenda kuandika kitabu chake.

 

Aidha, Profesa Tibaijuka akizungumzia suala la Virusi vya Corona, ameiomba Serikali kuangalia njia mbadala ikiwemo kutumia tiba za asili ili kuweza kukabiliana na ugonjwa huo kwa sababu hao wazungu wanaotuletea tiba zao sasa, hapo kabla walitukuta na tiba zetu za asili.

 

“Sisi lazima tuwe na mpango mbadala ambao unajikita kwenye jamii yetu, inabidi tuseme tiba zetu mbadala ziko wapi, hakuna jamii itakayokaa kusubiri kifo lazima itajihami.

 

“Tayari nimemuandikia barua Dkt. Ndugulile ya kwamba lazima tuangalie Plan B, nashukuru sana wananchi wa Muleba kwa kunipa nafasi kwa miaka 10 nimejifunza mengi, naenda kuandika kitabu,” alisema Profesa Tibaijuka.

Leave A Reply