The House of Favourite Newspapers

PROFILE: Usichokijua Kuhusu GODZILLA, Elimu, Muziki, Kifo! – VIDEO

Golden Jacob Mbunda ni kijana aliyezaliwa Januari 5, 1988 huko mkoani Morogoro.

Mbunda alifahamika zaidi kwa jina la Godzilla jina ambalo alilitumia sana kwa kazi zake za kisanii hasa katika tasinia ya muziki wa Bongo Flavor.

Godzilla alikuwa na kipaji cha uimbaji pamoja na kuandika nyimbo mbalimbali. Godzilla pamoja na ndugu zake wawili wa Damu katika malezi yao toka utoto wamelelewa na mama yao baada ya baba yao mzazi Jacob Mbunda kufariki Dunia wakati Godizilla akiwa na umri wa miaka miwili.

Mwaka 2007 Godzilla alishiriki katika mashindano ya freestyle ambapo hakufanikiwa kuibuka mshindi licha ya kuonesha uwezo mkubwa wa kuchana mistari.

Hata hivyo kushiriki kwake katika mashindano hayo kulimpa platform kubwa hasa katika tasnia ya muziki.

Comments are closed.