The House of Favourite Newspapers

PSG, Gor Mahia Wapewa Ubingwa

0

WAKATI Ligi mbalimbali zikisimama kutokana na kusambaa kwa virusi vya corona duniani, Ligi ya Kenya imemalizwa kwa ubingwa kupewa Gor Mahia huku Ufaransa ubingwa ukienda kwa PSG.

Kabla ya Ligi hiyo kumalizwa ilianza kusimamishwa kutokana na virusi hivyo na leo ndio wamefikia maamuzi hayo.
Wakati Kenya wakimaliza Ligi yao kwa kutoa ubingwa, Shirikisho la Soka Ufaransa (FFF) nao wametangaza kumaliza Ligi kwa kuwapa ubingwa PSG.

Licha ya kutanganza ubingwa, PSG, Marseille na Rennes watashiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao huku Lille, Reims na Nice wao watashiriki Ligi ndogo ya mabingwa Ulaya (Europa).

Maamuzi hayo pia ni habari nzuri kwa Ligi daraja la kwanza inayofahamika ‘Ligue 2’ kwa upande wa timu za Fc Lorient na Rc Lens ambao watakuwa Ligi Kuu msimu ujao wa 2020/21.

PSG wanachukua ubingwa huo wakiwa mbele kwa pointi 12, huku wakiwa na michezo mkononi baada ya kucheza mechi 27 katika ya 38.

 

PSG anaongza Ligi akiwa na pointi 68 katika michezo 27 huku nafasi ya pili, Marseille akiwa na pointi 56 katika michezo 28 wakati nafasi ya tatu akishikwa na Rennes wenye pointi 50 akicheza michezo 28.

 

Upande wa Gor Mahia wao wanachukua ubingwa huo wakiwa wanaongoza Ligi kwa pointi 54 katika michezo 23, nafasi ya pili ikishikiliwa na Kakamega Homeboys wenye pointi 47 michezo 22 na nafasi ya tatu ikishikiliwa na Tusker Fc yenye pointi 46 wakicheza pia michezo 22.

Huu unakuwa ni ubingwa wa tisa katika historia ya PSG kuchukua ubingwa wa ligi wakati Gor Mahia wenyewe ukiwa ni ubingwa wa 19 katika historia yao baada ya awali kuchukua mara 18.

Leave A Reply