The House of Favourite Newspapers

Putin, Zelensky na Biden Kukutana Uso kwa Uso Mkutano wa G20

0
Rais wa Indonesia Joko Widodo

RAIS mahasimu wanatarajiwa kukutana katika mkutano wa nchi 20 zenye uchumi mkubwa duniani G20 unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba mwaka huu.

 

Nchi ya Indonesia ambayo ndiyo mwenyeji wa mkutano kwa mwaka huu rais wake Joko Widodo amesisitiza kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin pamoja na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky lazima wote wahudhurie na kwa kutekeleza hilo Widodo ametuma mualiko kwa marais wote wawili mahasimu.

Rais wa Marekani Joe Biden

Kumekuwa na presha kutoka upande wa Marekani ambapo Rais wa Marekani Joe Biden ameshinikiza Urusi iondolewe kwenye mkutano huo huku akihitaji kuungwa mkono na mataifa mengine wanachama japo changamoto ya wazi ipo kwa taifa la China ambalo lenyewe limeshikilia msimamo wake wa kutokuunga uamuzi huo.

 

Naye Katibu wa Habari wa Ikulu ya Marekani Jane Psaki amesema:

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

“Rais amekwishaweka wazi kwa umma mtazamo wake kuhusu Rais Putin kuhudhuria mkutano wa G20, ni miezi sita kabla, kwahiyo hatujui hata namna ya kutabiri, hatuwezi kutabiri katika muda huu kwamba baadae itakuwaje tumeshawsilisha mtazamo wetu kwamba hatuoni kama wanatakiwa kuwa sehemu ya mkutano huo iwe hadharani au kwa siri.”

Kwa upande wake rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kupokea mualiko huo kwenye taarifa yake aliyoandika kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter ameandika:

 

“Nilikuwa na mazungumzo na Rais Jokowi, nashukuru kwa mualiko na msaada wako katika kupigania Uhuru na Usalama wa mipaka ya nchi, lakini hasa ikiwa ni sambamba na maadhimio ya Umoja wa Mataifa, tulijadiliana masuala ya Usalama na chakula, nashukuru sana kwa kunialika kwenye mkutano wa G20.”

Rais wa Urusi Vladimir Putin

Vita kati ya Urusi na Ukraine inaendelea ambapo zaidi ya watu milioni 5 weni wao wakiwa ni wanawake na watoto wakilazimika kukimbia makazi yao kujinusuru na madhara ya vita hiyo.

Leave A Reply