The House of Favourite Newspapers

Queen Mugesi Awa Miss Kinondoni 2019 (Picha +Video)

Miss Kinondoni 2019, Queen Mugesi Aynory (19)

USIKU wa kuamkia Julai 13 lilifanyika shindano la kumsaka Miss Kinondoni katika ukumbi wa Life Park Mwenge, ambapo mlimbwende Queen Mugesi Aynory (19) ameibuka kidedea na kuvaa taji lililokuwa linashikiliwa na Queenelizabeth Makune.

Mshindi wa pili alikuwa Prisca Kisunda, watatu Leila Adim wa nne Queen Anthony na wa tano ni Flaviana Sreven.

Queen Mugesi Aynory akiwa katika picha ya pamoja na na washitiki waliotinga tano bora.

Shoo ilivyokuwa

Awali alianza kupanda jukwaani msanii wa Bongo Fleva anayefahamika kwa jina la Bi. Aisha ambaye aliimba nyimbo kadhaa, kisha mshereheshaji (MC) aliwakaribisha washiriki wa Miss Kinondoni 2019 jukwaani kwa ajili ya kuwaburudisha wageni waalikwa sambamba na kuonesha mavazi yao.

Miongoni mwa mavazi yaliofunika usiku huo kwa washiriki ni pamoja na mavazi ya ubunifu, ufukweni na mwisho mavazi ya mtoko (usiku).

Washiriki wa Miss Kinondoni 2o19 waliotinga tano bora.

Baada ya hapo aliibuka jukwaani Miss Tanzania 2014, Lilian Kamazima kwa ajili ya kutaja kumi bora ambapo baada ya kumaliza warembo waliruhusiwa kuondoka.

Mobeto awabana 5 bora

Mchujo uliendelea na baada ya kupatikana tano bora, mwanamitindo na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto alipewa nafasi ya kuwauliza washiriki maswali kadhaa kabla ya kuipata tatu bora.

 

Amber Lulu

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Euggen ‘Amber Lulu’ naye alipewa nafasi ya kuimba nyimbo zake mara baada ya Mobeto kuwauliza maswali washiriki.

Amber Lulu aliwapagawisha washiriki na wadau waliofika kwa kuwapigia wimbo wake unaotikisa wa Jini Kisirani.

Washiriki wa Miss Kinondoni 2019 waliotinga 10 bora.

Tano bora hii hapa

Washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora katika usiku huo ni Prisca Kisuda, Queen Mugesi Aynory, Flaviana Steven, Leiya Adim na Queen Magesse.

Baada ya mchujo, ilipatikana tatu bora na walioingia ni pamoja na Queen Mugesi Aynory, Prisca Kisuda na Leiya Adim.

Hamisa Mobetto

Queen akutana na Queen

Historia ilijiandika kwa Queen wa 2018 kukutana na Queen wa 2019.

Queen Elizabeth alipanda jukwaani na kuvua taji lake kisha kumkabidhi Queen Mugesi kama Miss Kinondoni 2019 jambo lililoibua shangwe za kutosha ndani ya viwanja hivyo.

Apewa gari

Furaha ya Queen Mugesi haikuishia hapo kwani muda mchache baada ya kutangazwa rasmi kuchukua taji la Miss Kinondoni, alielekea sehemu iliyopo zawadi yake, ambapo muandaaji wa mashindano hayo Nancy Joseph alimkabidhi funguo ya gari aina ya Mini Cooper.

Mshindi wa pili sasa

Mbali na Queen Mugesi kukabidhiwa zawadi yake ya gari, naye mshindi wa pili, Prisca Kisuda alikabidhiwa samani za ndani ambazo ni kitanda chenye ukubwa wa futi tano kwa sita na mshindi wa tatu, Leiya Adim alipewa zawadi ya TV flat screen yenye ukubwa wa Inch 43.

Queen anena

Paparazi wa mtandao huu ambaye alikuwepo katika viwanja hivyo, alifanikiwa kuzungumza na Queen Mugesi na kufunguka kuwa alitarajia kushinda kwa sababu kwanza ana vigezo vyote vya kuwa mshindi japo changamoto zilikuwa ni nyingi ila anashukuru Mungu amepita.

“Unajua warembo tulikuwa wengi na kila mmoja alikuwa na uzuri wake, binafsi nilikuwa naamini nitashinda kwa sababu nina vigezo vyote ambavyo vilikuwa vinahitajika, nawaomba Watanzania waendelee kunisapoti kwani nina malengo ya kufika mbali zaidi ya hapa nilipofika.

Imeandaliwa na: Memorise Richard/GPL

 

Comments are closed.