The House of Favourite Newspapers

Raia wa Uganda Kuchagua Rais na Bunge Jipya Leo

0

 

Raia nchini Uganda wanapiga kura leo Januari 14, 2020 kuchagua rais mpya pamoja na wabunge katika uchaguzi mkuu utakuwa na ushindani mkali.

 

Vituo vya kupiga kura vinatarajiwa kufunguliwa saa moja asubuhi, saa za Afrika Mashariki, ambapo raia milioni 17.7 waliosajiliwa kama wapiga kura wanatarajiwa kushiriki hadi vituo vitakapofungwa saa kumi na moja jioni.

Usalama umeimarishwa huku wanajeshi wakipelekwa katika maeneo mbalimbali kushika doria.

Kwenye uchaguzi wa leo, kinyang’anyiro kikubwa ni kati ya rais wa muda mrefu Yoweri Museveni na mgombea wa upinzani ambaye pia ni mwanamuziki aliyegeukia siasa Robert Kyagulanyi maarufuku kama Bobi Wine.

 

Bobi Wine mwenye umri wa miaka 38, anawakilisha vijana wengi wa Uganda wenye ghadhabu wanaosema Rais Museveni mwenye umri wa miaka 76 na pia kiongozi wa zamani wa kivita, ni dikteta ambaye ameshindwa kukabili suala lililokithiri la ukosefu wa ajira na ongezeko la madeni ya umma.

 

Bobi Wine amekuwa karibu na wapiga kura vijana ambao ni sehemu kubwa ya watu nchini Uganda. Aghalabu vijana wengi wanaonekana kuukosoa utawala wa Museveni unaotuhumiwa kwa ufisadi. Bobi Wine anataka mabadiliko, kwa usaidizi wa mapinduzi ya amani.

Leave A Reply