The House of Favourite Newspapers

Rais Afungwa Jela Miaka 15

MAHAKAMA nchini Korea ya Kusini imemhukumu kifungo cha miaka 15 jela na kumwamru kulipa faini ya dola milioni 11.5 aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Lee Myung-bak (76) baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya rushwa.

 

Lee anakuwa Rais wa nne wa nchi hiyo kuhukumiwa kutumikia kifungo jela baada ya wengine watatu kufungwa kwa makosa ya rushwa akiwemo mtangulizi wake, Park Geun-hye ambaye alifungwa miaka 33 jela.

 

Mwanasiasa huyo ambaye aliingia madarakani Februari 25, 2008 hadi Februari 25, 2013, alithibitika kutenda kosa hilo wakati wa uongozi wake baada ya kupokea kiasi cha dola milioni 10 kutoka kwa kampuni ya Samsung na wakati wote wa kesi hiyo, Lee alikuwa akikana mashtaka hayo na kusema kuwa yamechagizwa kisiasa.

BREAKING: WAZIRI Jafo Awasha Moto Halmashauri Zilizofanya Vibaya

Comments are closed.