The House of Favourite Newspapers

Rais JPM Amtumbua Balozi; Asema Abebe Msalaba Wake – Video

0
RAIS John Magufuli  amemvua ubalozi na kumrejesha nyumbani aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Emilia Mkusa,  kutokana na ripoti  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali  (CAG) mwaka 2018/19 iliyoeleza upotevu na matumizi mabaya ya mabilioni ya fedha katika ubalozi huo.

 

Magufuli amesema hayo leo Alhamisi, Machi 26, 2020 baada ya kupokea ripoti ya CAG, Charles Kichere, na Ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

 

“Mmebaini wizi katika ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia na yule balozi nimeshamrudisha, siyo balozi tena kule. Itakuwa ni fundisho kwetu sisi kwamba ukiharibu mahali fulani ujiandae kubeba msalaba.

 

“Kwa mashirika kumi tu ya umma nkupongeza CAG umeokoa Shilingi bilioni 1.2; nakupongeza sana haiwezekani kazi yetu wenyewe tukaguliwe na watu wengine,” amesema Magufuli.

 

Awali akiwasilia ripoti hiyo Kichere amesema katika ukaguzi wake unaoishia Juni 30, 2019 amebaini Balozi za Tanzania nchini Brazil, Nigeria na Stockholm/Sweden zimetumia Sh1.02 bilioni kukodi nyumba za makazi,  kiasi hicho cha fedha kingeweza kuepukika kama balozi hizo zingekarabati nyumba zao za makazi.

 

Pia amesema katika ukaguzi wake amebaini kwamba balozi 14 za Tanzania zina majengo ambayo yametelekezwa, hivyo ameshauri majengo hayo kukarabatiwa ili kuokoa fedha ambazo zinatumika kukodi nyumba. Amezitaja baadhi ya balozi hizo kuwa ni pamoja na Canada, Burundi, Kenya, Sweden na Algeria.

 

Leave A Reply