The House of Favourite Newspapers

Rais Kenyatta Asaini Sheria ya Pedi Bure kwa Wanafunzi

RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesaini muswada wa sheria mpya ambayo sasa itakuwa sheria kamili, inayoitaka serikali kugawa pedi bure kwa wanafunzi wote wa kike nchini humo.

 

Kenyatta amesaini sheria hiyo jana Jumanne, Aprili 10, ambayo pia inaitaka serikali kuweka mazingira salama kwa wanafunzi hao kuweza kuhifadhi pedi zao.

 

“Sheria ya Marekebisho ya Elimu ya Msingi, kuweka wajibu wa kutoa taulo za usafi (pedi) za kutosha na za ubora kwa kila mtoto msichana aliyesajiliwa na kujiandikisha katika taasisi ya elimu ya msingi ya umma na kufikia ujira, kwa serikali”, imesema taarifa ya serikali ya Kenya.

 

Aidha, Ripoti ya UNESCO ya mwaka 2016 imeeleza kwamba binti mmoja kati ya 10 kwenye nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara, anakosekana shuleni kwa siku ambazo yupo kwenye hedhi, kutokana na kukosa pedi za kujistiri.

VIDEO; FUATILIA TUKIO HILO HAPA

Comments are closed.