
RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameungana na familia, ndugu, wasanii na waombolezaji wengine kuuzika mwili wa aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli aliyezikwa jana nyumbani kwao, Kiwangwa Bagamoyo, mkoani Pwani.

Mbali na Rais Kikwete, wengine waliofika ni Mwanaye ambaye pia ni Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, wasanii wakiwemo Rapa Fid Q, Roma, Snura Mushi, Ben Pol, G Nako na wengine.

Sam wa Ukweli alifariki dunia Jumatano usiku, Juni 6, 2018 katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu, na kuzikwa jana Ijumaa katika nyumbani kwao Kiwangwa, Bagamoyo.


Comments are closed.