The House of Favourite Newspapers

Rais Magufuli Ameagiza Ifakara Kuongezewa Kata na Halmashauri

Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Rais wa Tanzania, John Magufuli ameagiza Halmashauri ya mji wa Ifakara kuongezewa kata na halmashauri ya Wilaya ya Kilombero kubadilishwa jina.

Ametoa maelekezo hayo leo Jumapili Novemba 3, 2019 na kumtaka Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo kusimamia utekelezaji.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inaeleza kuwa Rais Magufuli amesema halmashauri hiyo iongezwe idadi ya kata kutoka halmashauri ya Wilaya ya Kilombero na makao makuu yake yawe Ifakara.

“Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero ibadilishwe jina iitwe halmashauri ya Wilaya ya Mlimba na makao makuu yawe Mgeta kama ilivyoamuliwa na baraza la madiwani, ” inaeleza taarifa hiyo.

Inaeleza kuwa kiongozi mkuu huyo wa nchi amewasisitiza viongozi wa halmashauri kutowayumbisha wananchi na watumishi kuhusu utekelezaji wa maelekezo hayo.

Comments are closed.