JPM Apokea Ripoti ya CAG Ikulu, Dodoma (Picha +Video)

RAIS John Magufuli leo Machi 26, 2020, amekabidhiwa Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2018/2019 iliyowasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere, katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu,  Chamwino, jijini Dodoma.

 

Pia amepokea Ripoti ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ya mwaka 2018/2019 iliyowasilishwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Brigedia Jenerali John Mbungo. 

Rais  Magufuli akipokea Ripoti ya Mwaka 2018-2019 kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere,  Ikulu ya Chamwino,  Dodoma leo Machi 26, 2020.

…Akisoma muhtasari wa taarifa ya  CAG.

…Akiangalia makabrasha mbalimbali aliyokabidhiwa na CAG.

…Akipokea Ripoti ya Mwaka 2018-2019 kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi  wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) Brigedia Jenerali John Mbungo.

  

…Akizungumza na viongozi mbalimbali mara baada ya kupokea ripoti  za  CAG na Takukuru. 

Brigedia Jenerali John Mbungo akisoma muhtasari wa taarifa yake.

…Rais  akiwa ameshika taarifa za CAG na Takukuru pamoja na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi  baada ya kuwakabidhi ili ya kuzifanyia kazi.

…Akizungumza  na  Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka kwenye ukumbi wa mikutano.

…Akiendelea kubadilishana mawazo na  Samia Suluhu na Kassim Majaliwa.

 

PICHA NA IKULU

Toa comment