The House of Favourite Newspapers

JPM Na Mkewe Washiriki Misa Katika Kanisa Katoliki La Mtakatifu Petro Dar – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakishiriki Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi, Novemba 17, 2019.

Rais  Magufuli akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) wakipeana mikono ya Amani na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wakati wa ibada ya Misa Takatifu.
Rais  Magufuli akisalimiana na Mtoto Cephas Kinunda mara baada ya ibada.
Rais Magufuli akiagana na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi na Mzee wa Kanisa Dkt. Adelhelm Meru mara baada ya ibada ya Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C”.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo Novemba 17, 2019 akiwa na mkewe Janeth Magufuli, Mama Marry Majaliwa (Mke wa Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa) pamoja na Waumini wengine wa Kanisa Katoliki wameshiriki Misa Takatifu Dominika ya 33 ya Mwaka “C” iliyofanyika katika kanisa la Mtakatifu Petro Parokia ya Oysterbay jijini Dar es Salaam. Ibada iliyoongozwa na Paroko wa parokia hiyo Padre Dkt. Alister Makubi, Novemba 17, 2019.

Comments are closed.