The House of Favourite Newspapers

Rais wa Senegal Amteuwa Kiongozi wa Upinzani Ousmane Sonko kuwa Waziri Mkuu

0

RAIS mpya wa Senegal, Bassirou Diomaye Faye, amemteuwa kiongozi maarufu wa upinzani Ousmane Sonko, kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo, baada ya kuapishwa kuwa Rais rasmi.

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Oumar Samba Ba, ametangaza uteuzi huo wa Sonko kupitia agizo la Rais lililopeperushwa kwenye kituo cha televisheni cha umma RTS.

Akizungumza baada ya kuteuliwa kwake, Sonko amesema kuwa atawasilisha kwa Rais orodha kamili ya mapendekezo ya uteuzi wa mawaziri ili kuidhinisha.

Sonko ameongeza kuwa hatamuacha Rais kukabiliana na jukumu hilo zito peke yake.

RAIS SAMIA AKIZINDUA TUME YA ULINZI WA TAARIFA BINAFSI MUDA HUU – JNICC, DAR ES SAALAM

Leave A Reply