The House of Favourite Newspapers

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete akiwa shambani kwake Msoga mkoa wa Pwani

0

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa shambani kwake kijijini Msoga mkoa wa Pwani kukagua upandaji wa mahindi na majani ya malisho ya mifugo.

Dkt. kikwete, ambaye ni mkulima na mfugaji mashuhuri kijijini hapo, hutumia wakati wake mwingi shambani hapo toka astaafu, huku katika muda mwingine, mbali ni kutumikia taasisi kadhaa za kimataifa ikiwemo Taasisi ya Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) ambayo yeye ni mwenyekiti, pia anaendesha Taasisi yake ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation iliyojikita katika kusaidia juhudi za serikali kuboresha afya ya uzazi, mama na mtoto na vijana.

 

Leave A Reply