The House of Favourite Newspapers

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Afungua Mkutano Wa Wa Pili Wa Kisayansi Wa Afya Ya Uzazi Na Mtoto Ukumbi Wa Mikutano Wa Julius Nyerere Jijini Dar

0
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifungua Mkutano wa Pili wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Kijana, na Lishe (RMNCAH+N) katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julis Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam chini ya kauli mbiu: “Kukuza upatikanaji wa Huduma Bora za Uzazi, Mama na Mtoto, Kijana”.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefungua Mkutano wa Pili wa Kisayansi wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto, Kijana, na Lishe (RMNCAH+N) katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julis Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam Novemba 15, 2023 chini ya kauli mbiu: “Kukuza upatikanaji wa Huduma Bora za Uzazi, Mama na Mtoto, Kijana”.

Dkt. Kikwete pia alitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho yaliyoandaliwa na wadau wa afya.

Mkutano huo, utakaofanyika hadi Novemba 17, 2023 umeandaliwa na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa kushirikiana na washirika kadhaa ikiwa ni pamoja na taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), unahudhuriwa na watu wapatao 2,800 kutoka makundi ya wadau mbalimbali wa afya wa ndani na wa kimataifa.

Wazo la kufanyika kwa mkutano huo kwa mara ingine lilizaliwa katika moja ya mikutano ya kawaida ya kila robo ya Kikundi Kazi cha Kiufundi cha RMNCAH+N kwa lengo la kuleta wadau muhimu pamoja ili kusambaza, kuthibitisha, na kujifunza mafundisho yanayopatikana kwa vitendo bora na hatua za msingi zinazotokana na ushahidi wa kisayansi ili kuhakikisha utekelezaji bora.

Leave A Reply