The House of Favourite Newspapers

Rais Ruto Aidhinisha Ongezeko la Ushuru Kenya

0
Rais wa Kenya William Ruto.

Rais wa Kenya William Ruto ametia saini kuwa sheria mswada wa kwanza wa fedha wa serikali yake, unaolenga kuongeza mapato kwa kutoza kodi katika bidhaa kadhaa bila kujali ukosoaji kwamba ongezeko hilo la kodi litasababisha matatizo mengi zaidi ya kiuchumi kwa wananchi.

Moja ya mabadiliko yenye utata yaliyopitishwa na bunge wiki iliyopita ni kuongeza mara mbili zaidi ushuru wa ongezeko la thamani utakaotozwa kwenye mafuta kwa asilimia 16 kutoka asilimia 8.

Wafanyakazi wa serikali pia watatoa asilimia 1.5 ya mishahara yao kwa ajili ya malipo ya nyumba ambayo yatakwenda kwenye mpango ambao utalipia kujenga nyumba kwa ajili ya watu wenye kipato cha chini.

“Rais Ruto ameidhinisha mswada huo wa fedha. Umetiwa saini Ikulu,” ofisi ya rais ilisema katika ujumbe wake kwa waandishi wa habari, ulioandamana na picha za Rais Ruto akitia saini waraka huo.

Ruto, ambaye alichukua wadhifa mwezi Septemba baada ya uchaguzi uliokuwa na upinzani mkubwa, anajaribu kuongeza fedha kwenye hazina ya serikali iliyoporwa na kukarabati uchumi wenye madeni makubwa aliourithi kutoka kwa Rais aliyemtengulia Uhuru Kenyatta, ambaye alitumia pesa nyingi katika miradi mikubwa ya miundombinu.

Sheria mpya — inatarajiwa kuzalisha zaidi ya dola bilioni 2.1 – kwa kuongeza kodi za bidhaa na huduma za msingi, ikiwa ni pamoja na chakula na m fumo wa kutuma pesa kwa simu.

Katika ongezeko hilo la kodi, watu wanapokea msahara wa shilingi 500,000 kwa mwezi, sasa watalipa asilimia 32.5 ya kodi ya mapato wakati wale wanaopokea shilingi 800,000 watalipa asilimia 35 ya kodi kutoka asilimia 30 wanayolipa sasa.

Kodi ya mauzo kwa biashara ndogo ndogo pia imeongezeka mara tatu kufikia asilimia tatu.

 

Leave A Reply