The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aagiza Benki Kushusha Riba (Picha +Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akivuta utepe pamoja na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga kufungua Jengo la Ofisi ya Benki Kuu ya Tanzania tawi la Mwanza katika sherehe zilizofanyika Jijini Mwanza leo.

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameiagiza Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kushusha viwango vya riba vinavyotozwa na benki mbalimbali, angalau ziwe chini ya asilimia 10.

Rais Samia ametoa maagizo hayo leo, Juni 13, 2021, wakati akifungua jengo la Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Mwanza.

Amesema, hatua hiyo itapunguza machungu kwa wananchi ambao wamekuwa wakikutana na viwango vikubwa vya riba hivyo kuchelewesha maendeleo. 

“Benki Kuu iangalie riba isiwe inayomuumiza mwananchi, kwani zipo juu na naelekeza zianze kushushwa na kama mfumo una matatizo ushughulikiwe angalau uwe kuanzia asilimia 10 kwenda chini,” amesema Rais Samia.

Katika kusisitiza hilo, Rais Samia amesema; “BoT iweke mikakati ya kuhamisha na kuweka mazingira rafiki ya kutoa mikopo.”

Pia, ameelekeza Benki Kuu, ikaelekeze nguvu katika kuhamisha matumizi ya mtandao ili kupunguza matumizi ya pesa taslim kwa kuwa itarahisisha biashara, makusanyo ya mapato na uchapishaji wa pesa.”

Rais Samia, ameagiza kuwepo kwa kanzidata mbili za kutunza taarifa ya kwao yenyewe na nyingine itunzwe kwingine ili moja inapoleta shida nyingine, inafanya kazi.

“Nashauri BoT mshirikiane na wadau wengine ikiwemo wizara ya teknolojia ya habari, kuona jinsi ya kupata huduma hii kwa gharama nafuu,” amesema

Katika uzinduzi huo, Rais Samia ameshtushwa na gharama za ujenzi wa jengo hilo lililogharimu shilingi bilioni 42 ikiwa ni ghama za ujenzi na ufungaji wa vifaa vikiwemo vya ulinzi.

“Naipongeza sana Benki Kuu kwa jengo hili la kisasa, lakini ujenzi wa majengo haya gharama kidogo, zimesisimua mishipa ya fahamu, tutalitizama zilivyokwenda, leo ni uzinduzi na tutaulizana zimetumikae baadaye,” amesema.

 

Awali, Gavana wa BoT, Profesa Florens Luoga amesema, kwa sasa benki hiyo, ina matawi manne; Mbeya, Mwanza, Mtwara na Arusha huku ikiwa na ofisi ndogo Dar es Salaam na Zanzibar. Makao Makuu yamehamia Dodoma kuanzia Novemba 2020.

 

Amesema, ujenzi wa ofisi hizo ulifanyika kutokana na kupanuka kwa majukumu ya BoT Kanda ya Ziwa na bodi ya wakurugenzi waliithinisha ujenzi wa jengo hili ambao ulianza Juni, 2015 na kukamilika Oktoba, 2020.

 

Amesema, baada ya kupitia ujenzi wa jengo, kulionekana kuna haja ya kuongeza ulinzi na kuanzia Aprili, 2021, walianza kuhamishia ofisi humo.

 

“Ujenzi umegharimu shilingi bilioni 42.1 ikiwemo ufungaji wa vifaa mbalimbali ikiwemo mitambo ya usalama na mawasiliano,” amesema Profesa Luoga.

Gavana huyo amesema, BoT imekuwa inakutana na changamoto kadhaa ikiwemo matumizi makubwa ya pesa taslim katika kufanya miamala.

STORI NA SIFAEP PAUL | GPL

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP:

⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8

⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply