The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Aeleza Mlima Kilimanjaro Ulivyopoteza Barafu “Hatujasalimika” – Video

0

RAIS Samia Suluhu Hassan, ameyataka mataifa makubwa yanayozalisha kiwango kikubwa cha hewa ya ukaa inayochafua mazingira, kuwa mstari wa mbele kutekeleza program mbalimbali za kutunza mazingira, ikiwa ni pamoja na kutoa misaada na mikopo nafuu kwa nchi zinazoendelea ili zitekeleze kwa ufanisi miradi ya utunzaji wa mazingira.

 

Rais Samia ameyasema hayo jijini Glasgow, Scotland wakati akituhubia katika Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa unaojadili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (COP26) na kuongeza kuwa Tanzania imeathirika vibaya na mabadiliko hayo ikiwa ni pamoja na kukumbwa na majanga kama mafuriko na ukame.

 

Ameongeza kuwa licha ya hatua thabiti zinazochukuliwa na serikali, lakini majanga ya asili yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, yanaendelea kutokea ikiwemo kuongezeka kwa kina cha bahari pamoja na kuyeyuka kwa theluji katika Mlima Kilimanjaro.

 

Sisi Tanzania hatujasalimika na majanga haya. Kupanda kwa kina cha maji kunachukua ardhi yenye rutuba, fahari yetu Mlima Kilimanjaro unabaki mtupu kwa kuyeyuka kwa barafu na tunakumbwa na mafuriko na ukame usiotabirika.

 

Mabadiliko ya tabianchi yanamaanisha 30% ya Pato la Taifa la Tanzania ambalo linatokana na kilimo, misitu na uvuvi liko hatarini. Cha kusikitisha ni kuwa mikakati mikubwa ya kukabiliana na vyanzo na athari zake haijapewa uzito.

 

Lengo la [Makubaliano ya] Paris la kufikia 1.5°C halijafikiwa, lakini bado makubaliano zaidi yanawekwa. Tunachotakiwa wote kukumbuka ni kwamba mabadiliko makubwa ya tabianchi yatakapotukumba hayatachagua eneo, imara au dhaifu, nchi tajiri au maskini. Muda wa kuchukua hatua ni sasa,” amesema Rais Samia Suluhu.

 

Leave A Reply