The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Afanya Uteuzi Mpya Jioni Hii

0

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali ambapo amemteua Prof. John Kondoro kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) baada ya kumaliza muda wa kipindi cha kwanza, uteuzi huu umeanza April 15, 2021.

 

Rais amemteua Dkt. Richard Masika kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) akichukua nafasi ya Marehemu Prof. Peleka ambaye alifariki dunia, uteuzi huu umeanza April 16, 2021.

 

 

Rais amemteua Prof. Joseph Msambichaka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) akichukua nafasi ya Prof. Manase Salema, uteuzi huu umeanza Aprili 15, 2021.

 

 

Rais amemteua Prof. Makenya Maboko kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), amemteua pia Ernest Mihayo kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Bahari Dar es Salaam, baada ya kumaliza muda wa vipindi vyao vya kwanza.

 

 

Rais amemteua Prof. Esther Lugwisha kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Mkemia Mkuu wa Serikali baada ya kumaliza kipindi cha kwanza.

 

 

Rais amemteua Dkt. Revocatus Mushumbusi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ladislaus Nshumbemuki ambaye amestaafu.

 

 

Rais amemteua Dkt. Mboni Ruzegea kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (TLSB) akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Ali Mcharazo ambaye amestaafu.

 

Leave A Reply