The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Akamilisha Mradi Wa Maji Kigoma Mjini Bil.42 Chanzo Cha Ziwa Tanganyika

0

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso ametembelea na kukagua chanzo kipya cha maji cha Amani beach, ziwa Tanganyika chenye chenye uwezo wa kuzalisha lita za maji milioni 42 kwa siku.

Waziri Aweso akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Kigoma

Mradi huu una thamani ya Tsh. bilioni 42 ukiwa umekamilika kwa asilimia mia moja.
Mradi huu umekua ni faraja kubwa sana kwa wana Kigoma mjini kutokana na ugumu wake katika hatua za ujenzi.

 

Baada ya ukaguzi na kujionea hatua ya ukamilikaji wa Mradi, Waziri Aweso amefanya kikao kikubwa cha ndani na viongozi wadau wa Maji Kigoma kilichohudhuriwa na Waheshimiwa wabunge mkoa wa Kigoma, Mkuu wa mkoa, Mkuu wa Wilaya Kigoma mjini, Mkurugenzi, Katibu Tawala Mkoa na Wilaya, Waheshimiwa madiwani, Kamati ya Siasa CCM Mkoa ,Kamati ya siasa CCM Wilaya, Wadau wa vyama vya siasa, Watendaji wote wa kata 19 za Manispaa ya Kigoma Ujiji, Maafisa Tarafa, wenyeviti wa serikali za mitaa za Manispaa ya Kigoma Ujiji, watendaji kata, Viongozi mbalimbali wa chama na serikali, viongozi wa dini, na wadau wa Maji.

Waziri Aweso akikagua baadhi ya miundombinu ya mradi wa maji, Kigoma

 

Katika kikao hicho, Waziri Aweso amefikisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan na pongezi kwa wana Kigoma mjini kwa kukamilisha ujenzi wa Mradi huu wa Kihistoria ambao chanzo chake ni Ziwa Tanganyika.

Wadau mbalimbali waliohudhuria kikao hicho, wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia kwa kutekeleza kwa vitendo dhamira ya kumtua Mama ndoo kichwani.

 

Katika hatua nyingine akizungumza katika kika hicho Waziri Aweso amesema Rais Samia atakuja kuzindua mradi huu wakati wowote na kuelezea kuwa mradi hii tayari umezifikia kata zote 19 na kazi inayoendelea sasa ni usambazaji na ili kuwafikishia wananchi Maji majumbani na maeneo ya pembezoni na kuboresha na kuimarisha huduma ya maji.

Leave A Reply