The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Ashiriki Uzinduzi wa Filamu ya The Royal Tour – JNICC, Dar (Picha +Video)

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour uliofanyika katika Ukumbi wa Julius Nyerere Conventional Centre Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Mei, 2022

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameshiriki katika uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour katika Ukumbi wa JNICC, jijini Dar es Salaam leo tarehe 08 Mei, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango, Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla, Mwenyekiti wa Kamati ya Royal Tour Dkt. Hassan Abbas pamoja na viongozi mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wakitazama Filamu ya Tanzania The Royal Tour katika ukumbi wa Julius Nyerere Conventional Centre tarehe 08 Mei, 2022
Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa pamoja na Wageni mbalimbali wakiwa katika uzinduzi wa Filamu ya Tanzania The Royal Tour katika ukumbi wa Julius Nyerere Conventional Centre tarehe 08 Mei, 2022
Wajumbe wa Kamati ya Tanzania The Royal Tour wakifurahia Tuzo yao waliokabidhiwa na Bodi ya Filamu na Shirikisho la Filamu Tanzania kutokana na kazi kubwa waliofanya wakati wa utengenezaji na Utangazaji wa Filamu hiyo ya Tanzania Royal Tour
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makalla pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Tanzania The Royal Tour Dkt. Hassan Abbas mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Julius Nyerere Conventional Centre Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Filamu ya hiyo tarehe 08 Mei, 2022

PICHA NA IKULU

 

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply