The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Akutana na Ugeni Huu Ikulu

0

RAIS Samia Suluhu Hassan leo Julai 27, 2021 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Africa (Africa CDC, Dk. John Nkengasong ikulu jijini Dar es Salaam.

 

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Jaffar Haniu, inaeleza kuwa Dk. Nkengasong amempongeza  Rais Samia kwa hatua mbalimbali anazozichukua katika kukabiliana na Ugonjwa wa Corona na kusema kuwa kituo hicho kinaunga mkono jitihada hizo za serikali.

 

Amesema kituo hicho kimedhamiria kushirikiana na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) katika kuweka mipango ya pamoja na kutumia fursa zinazopatikana kupitia kituo hicho katika mapambano dhidi ya Corona ikiwa ni pamoja na upatikanji wa chanjo na usambazaji wake.

 

Kwa upande wake, Rais Samia amemshukuru Dk. Nkengasong kwa kuitembelea Tanzania na kueleza kuwa serikali ipo tayari kufanya kazi na wataalamu kutoka Africa CDC katika kukabiliana na ugonjwa huo na kuongeza kuwa serikali inakusudia kujenga viwanda vya kuzalisha chanjo za aina mbalimbali katika kukabilianana magonjwa ya mlipuko.

Leave A Reply