The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Asisitiza Haki kwa Wananchi – Video

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka majaji na mahakimu kuhakikisha wanasimamia haki ili wananchi wanyonge waliodhulumiwa haki zao wanazipata.

 

Rais Samia amesema hayo leo Oktoba 6, 2021 wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa Jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki katika eneo la National Capital City, Jijini Dodoma.

 

“Mafanikio hayawezi kupatikana endapo wasimamizi na wadau wa mfumo wa utoaji haki nchini hawatafanya kazi zao kwa kuzingatia sheria, taratibu na kuongozwa na nafsi katika kufanya kazi na maamuzi.

 

“Tumesikia idadi kubwa kata na tarafa ambazo hazina makahama na kwa kweli ni kunyima haki wananchi kwahiyo Serikali na wadau tutaangalia tutajitahidi kuhakikisha tunafika kwenye maeneo hayo.

 

“Pamoja na ujezi wa vituo jumuishi vya utoaji wa haki, kuongeza idadi ya majaji na mahakimu, kuanzisha mahakama zinazotembea na kuimarisha matumizi ya Tehama hatuwezi kupata mafanikio endapo mahakimu, majaji hawataongozwa na roho njema katika utoaji wa haki.

 

“Tuhakikishe haki kwa wananchi inapatikana vile inavyopaswa pia ninatoa rai kwa mahakama kushughulikia suala la ucheleweshwaji wa kesi. Niwasihi sana mlipe kipaumbele suala la kusikiliza kesi haraka, msikubali kirahisi kubadilisha mahakimu au tarehe za kusikiliza kesi kwasababu hii ni moja ya sababu inoyosababisha kesi zichelewe.

 

“Niwaombe sana Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi muangalie usimamizi wa ubora wa maamuzi kwenye mahakama za mwanzo, malalamiko mengi ya mahakama yanahusu mahakama za mwanzo, kule kutupiwe jicho vizuri,” amesema Rais Samia.

 

Leave A Reply