The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Atekeleza Mradi Wa Maji Bil.35 Kasulu Mjini

0

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akiwa Kasulu mjini mkoani Kigoma ametoa salam na kupokea shukrani za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa wananchi waliojitokeza kushuhudia tukio la kihistoria la kuanza kwa ujenzi mkubwa wa Maji utakaomaliza kabisa changamoto ya Maji Kasulu mjini.

Waziri Aweso akisalimiana na viongozi, Kasulu Mjini

 

Aidha, Waziri Aweso akiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Prof Joyce Ndalichako ambae pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, vijana, Ajira na wenye Ulemavu amemtambulisha rasmi na kumkabidhi eneo la mradi Mkandarasi wa mradi wa Miji 28 Kwa mji wa Kasulu.

 

Mkandarasi huyo ambaye ni Megha Engineering and Infrastructures Ltd atajenga chanzo cha maji, mtambo wa kutibu maji wenye uwezo wa Lita milioni 15, matenki mawili ya jumla ya ujazo wa Lita milioni 2 pamoja na mtandao wa usambazi maji katika Kata zote 8 za mji wa Kasulu. Gharama ya mradi ni shilingi bilioni 35, Mkandarasi ameshalipwa malipo ya awali, mradi umeanza rasmi tarehe 11 Aprili 2023 na utatekelezwa Kwa muda miezi 30, unategewa kukamilika tarehe 10 Oktoba, 2025.

 

Wananchi wa Kasulu Mjini wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo wamemshukuru kwa dhati Mheshimiwa Rais Samia kwa kutekeleza kwa vitendo ahadi ya kumtua Mama ndo kichwani kwani sasa Kasulu mjini inakwenda kupata Maji ya uhakika, yalio safi, Salama na yenye kutosheleza.

Mradi huu ukikamilika utahudumia zaidi ya wakazi 224,000 na kukidhi kusambaza maji Kwa mji wa Kasulu Kwa asilimia mia.

Leave A Reply