The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Atunukiwa Shahada Ya Heshima Ya Udaktari Wa Falsafa, India – Video

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru Profesa Santishree Dhulipudi Pandit kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023. Rais Samia ni Mwanamke wa Kwanza kutunukiwa Shahada hiyo ya Heshima na Chuo hicho nchini India. Ni Viongozi wawili tu ambao wametunukiwa Shahada hiyo ya Heshima akiwemo Rais wa Urusi. Vladmir Putin pamoja na Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Japan Hayati Shinzo Abe

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 10, 2023 ametunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawarhalal Nehru, Delhi India.

Ametunukiwa PhD hiyo kwa mchango wake kwenye diplomasia ya uchumi, kuwa chachu ya maendeleo yanayogusa wananchi moja kwa moja na mchango wake kuimarisha uhusiano wa kimataifa.

Mara baada ya kutunukiwa shahada hiyo, Rais Samia ameitunuku kwa mabinti wa Tanzania wanaoishi katika mazingira magumu.

Anawasihi kujituma ili kufikia malengo yao kwani jitihada huzaa matunda mazuri.

Tangu kuingia madarakani Rais Samia ameweka jitihada kusaidia watoto wakike ikiwa ni pamoja na kuruhusu wanafunzi waliojifungua kuruhusiwa kuendelea na masomo.

Hii ni shahada ya kwanza ya udaktari kwa Rais Samia kutunukiwa ugenini na ya kwanza kutolewa kwa mwanamke na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru.

Leave A Reply