The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Awabadilisha Kafulila na Mongella – Video

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amembadilisha John Mongella kutoka kuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu na kwenda kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha. 

 

Samia amesema hayo leo Jumatano, Mei 19, 2021 wakati akihutubia mara baada ya kumaliza kuwaapisha wakuu wa mikoa na wakuu wa taasisi, Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

“Kuna mabadiliko madogo nimefanya, Kafulila nilimteua kuwa RC Arusha na Mongella kuwa RC Simiyu, nimeamua Mongella kwa sababu ulikuwa unaongoza Mkoa mkubwa basi ukawe RC Arusha na Kafulila kwa sababu ndio anaanza alikuwa RAS basi akawe RC Simiyu.

 

Wote mlioapa na mlioteuliwa hongereni sana, nasema hongereni kwasababu Tanzania kuna Watu wengi na 15% wangefaa kuteuliwa lakini mmeteuliwa nyinyi, naamini mnapokwenda kufanya kazi zenu mtasimama na Mungu.

 

Baada ya shughuli hizi za kuapishana na kupiga picha Wakuu wa Mikoa na Wateuliwa wengine mtarudi hapa na tutakuwa na kikao cha kazi kwahiyo kwasababu nina mambo mengi ya kuongea na nyinyi leo tuishie hapa tutakutana kwenye kikao cha kazi,” amesema Samia.

 

Kabla ya kuteuliwa kwenda Simiyu Mongella alikuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza. Awali David Kafulila alikuwa Katibu Tawala Mkoa (RAS) wa Songwe kabla kwenda kugombea Ubunge, aliteuliwa kuwa RC Arusha sasa amepelekwa Simiyu.

 

Leave A Reply