The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Kukutana na Wazee wa DSM Kesho

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kesho Ijumaa ya Mei 07, anatarajiwa kufanya mkutano na zaidi ya Wazee 900 wa Mkoa wa Dar es salaam ambapo Katika kikao icho watajadili mambo mbalimbali.

 

Akitoa taarifa ya mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amesema kikao icho kitafanyika Ukumbi wa Mikutano Mlimani City kuanzia saa 8 mchana.

 

Aidha RC Kunenge ametoa wito kwa Wazee waliopata mialiko ya kushiriki kikao icho kujitokeza kwa wingi ili wapate kusikiliza kile ambacho Rais Samia amewaitia.

 

Kwa upande wao Viongozi wa Wazee wamemshukuru Rais Samia kwa kuona umuhimu wa kukutana na Wazee huku wakisema wanatarajia kikao icho kitakuwa na manufaa makubwa kwao.

Leave A Reply