The House of Favourite Newspapers

Rais Samia Mgeni Rasmi Tamasha la Utamaduni

0

RAIS Samia Suluhu Hassan, kesho Septemba 7, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la siku mbili la utamaduni wa Mtanzania litakalofanyika katika eneo la Kituo cha Utamaduni Bujora Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, Katibu wa Umoja wa Machifu wa Kisukuma, Aaron Mikomangwa, amesema tamasha hilo litakusanya machifu zaidi ya 120 kutoka katika sehemu mbalimbali nchini pia litahusisha maonyesho ya vyakula vya asili, michezo ya jadi na mambo kadha ya mila na desturi.

 

“Kutakuwa na mafundisho na mafunzo mbalimbali ya kimila ikiwemo namna na taratibu za kuwasimika viongozi wa jadi madarakani,” amesema Mikomangwa.

 

Leave A Reply