Rais Samia: Mtetezi Pekee wa Haki za Binadamu Tanzania ni Katiba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo amehudhuria hafla maalum ya maadhimisho ya miaka 10 ya kukuza, kutetea watetezi wa haki za Binadamu na nafasi za kiraia nchini Tanzania uliofanyika katika Ukumbi wa PSSSF Dar es Salaam.

 

Katika hotuba yake Rais Samia amesema Tanzania kama nchi inazo sera na sheria mbalimbali zinazolinda haki na uhuru wa mwanadamu ambazo zipo tangu kuasisiwa kwake kwenye Azimio la Arusha mwaka 1967 ambalo lilizingatia tamko la Umoja wa Mataifa la haki za binadamu la mwaka 1948.

 

Rais Samia amewataka watetezi wa haki za binadamu kutumia fursa kuwaelemisha wananchi juu ya kufuata na kuielewa Katiba kwani kwenye Katiba ndiko kunakopatikana haki na wajibu.

Wahudhuriaji kwenye maadhimisho ya miaka 10 ya kukuza, kutetea watetezi wa haki za Binadamu na nafasi za kiraia nchini Tanzania

“Mtetezi mkubwa wa haki za binadamu ndani ya Tanzania ni Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo Serikali ndiyo inaitekeleza ndiyo sheria mama ambayo ina haki zote za wanadamu wanaoishi Tanzania swala langu kwenu je hawa wanadamu tunaowatetea wanaijua hiyo katiba? Na nataka niache kazi kwenu.”

 

Rais Samia amewaasa watetezi huo kujikita zaidi katika kutetea matukio mbalimbali ya kijamii hasa ikiwemo ubakwaji wa watoto na unyanyasaji wa kijinsia kuliko kujikita zaidi katika katika kuwatetea wanasiasa.701
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment