The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Soko Jipya Kujengwa Karume

0

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itajenga Soko jipya la Karume ambapo walikuwa wakifanya biashara zao na kujiingizia kipato.

 

Rais Samia amesema hayo leo Jumanne, Januari 25, 2022, wakati akizungumza na viongozi wa wamachinga Ikulu Dar es Salaam na kuongeza kuwa Serikali inawatambua rasmi machinga kama kundi maalum, na litakuwa moja ya Makundi yatakayohudumiwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Makundi Maalum.

 

“Juzi nilipokutana na RC Makalla nilimwambia nendeni wekeni mipango mizuri Karume lakini acha wamachinga warudi haraka Karume, niliamua hivyo kwasababu nilijua mkiwa nje mambo yatasimama, hata kama tuna mipango ya kujenga masoko ya kisasa lakini kwa sasa muendelee na biashara.

 

“Nimetoa pesa nyingi tu la Kujenga Soko la Kariakoo, pia nimemuambia RC Makalla aanze kutafuta Mkandarasi tujenge soko Jangwani fedha tayari zipo, baada ya Jangwani tutajenga Karume, lazima kuwe na masoko katikati ya Jiji ambayo yatafanya kazi saa 24 yenye huduma zote.

 

“Miongoni mwa changamoto mlizozisema wamachinga ni ukosefu wa mitaji na Makamu Mwenyekiti hapa alikuwa na uhakika kwamba kwenye fedha za Uviko 19 kuna Bilioni tano zenu, nitakaa na TAMISEMI tuone mipango yao wameiwekeaje lakini niwaahidi kati ya Bilioni 5 zitatoka fedha za kuongeza nguvu kwenye SACCOS yenu.

 

“Niwadokeze sio tu fedha za Uviko nimewaelekeza Mabenki yaje ya programu maalumu zitakazosaidia Wanawake au Vijana na sitozisema hadi wenyewe wazizindue, katika programu hizo tutaangalia jinsi wamachinga mtakavyoweza kukopa kwenye Mabenki kwa njia nafuu sana kwa ile mipango watakayokuja nayo, kwahiyo tutahakikisha Saccos za Wamachinga tunazitunisha mpaka zinakuwa Taasisi zinazojitegemea,”  amesema Rais Samia.

Leave A Reply