The House of Favourite Newspapers

Rais Samia: Vijana Wengi Wanahangaika na Supu ya Pweza, Vumbi la Kongo -Video

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala pamoja na Watumishi wa Serikali mara baada ya kuweka saini Mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo Mtumba Mkoani Dodoma tarehe 30 Septemba, 2022.

RAIS Samia leo Ijumaa Septemba 30, 2022 ameagiza kufanyika utafiti wa kwanini vijana balehe wanamatizo ya lishe ili kuepuka kuwa na Taifa goigoi. Samia ameyasema hayo wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamiaji shughuli za lishe.

Amesema wakati wakutafuta watoto vijana hao wanahangaika mara kunywa supu ya pweza na kwamba kuna tatizo ambalo wanalijua lakini wanalificha.

 

“Watafiti fanyeni tafiti, tuna tatizo, kwasababu halisemwi ni siri linawaumiza zaidi vijana wetu, mara haya ninayoyataja, mara vumbi la Kongo, mara kitu gani lakini tatizo kubwa liko kwenye lishe. Sasa watafiti fanyeni tafiti vijana wetu waweze kuzaa watoto wenye afya,”amesema Rais Samia.

Wakuu wa Mikoa wakiwa kwenye hafla ya uwekaji wa saini mikataba ya Usimamiaji wa Shughuli za Lishe, Mtumba Jijini Dodoma tarehe 30 Septemba, 2022.

Amesema jamii hiyo ni ya watu wote waweze kufanyia kazi na kwamba wakiacha hilo liendelee wanaenda kuwa na Taifa goigoi ambalo lina watu lakini si raslimali watu ambao ni mzigo kwa Taifa na si wazalishaji kwa ajili ya Taifa.

 

“Tutafika mahali hatujui mume nani, mke nani. Kwa hiyo twendeni tukasimamie hilo…Wavulana mnaonekana mmevaa suti lakini kuna vigenge vya udongo (vumbi) la kongo chungu mzima, Amos (Mkuu wa Dar es Salaam-Amos Makala) unanitazama huko ndio kunasifika kwa chipsi,”amesema

Leave A Reply