The House of Favourite Newspapers

Rais Ukraine Akiri ‘Hali Tete’ Kuwanusuru Askari Wake Waliozingirwa na Urusi Mariupol

0
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

 

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amethibitisha kuwepo kwa ugumu wa mazungumzo ya namna ya kuwaondoa askari majeruhi katika eneo lililozingirwa na kushambuliwa na Urusi, huko Mariupol.

 

Akizungumza kuhusu hali ilivyo Azovstal, Mariupol alieleza kuwa askari waliosalia wa Ukraine wanaopambana kulinda mji huo na ambao wengi wao wamejeruhiwa wanahitaji kuondolewa katika eneo hilo kwa ajili ya matibabu.

Mji wa Mariupol ulioko Kusiku mwa Ukraine, ni mji muhimu kwa Urusi kimkakati, Urusi wamekuwa wakielekeza nguvu zao na kuushambulia askari wa Ukraine wanaoulinda ili kuuteka kwa miezi kadhaa sasa.

 

Zelensku anakiri mazungumzo ya namna ya kuwaondoa ni magumu.

“Majadiliano tata yanaendelea katika hatua nyinginre yenye lengo la kuwaondoa waliojeruhiwa vibaya,” alisema.

 

“Tunafanya kila liwezekanalo kuwaondoa wote, kila askari wetu mlinzi,” amesema Zelensky.

Ameongeza kuwa Kyiv imekuwa ikitumia “wapatanishi wenye ushawishi” katika mazungumzo hayo, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Leave A Reply