The House of Favourite Newspapers

Rais wa Botswana Kufanya Ziara Nchini-Video

0
                                 Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi

 

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula, amesema kuwa Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi atawasili kesho Tanzania Juni 9, 2021.

Ameeleza kuwa Rais Masisi atakuwa Tanzaniakwa ziara ya siku mbili ya kikazi kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

“Viongozi wetu wanatarajia kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, uhusiano wa kidiplomasia, matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini Botswana, bishara na uchumi pamoja na namna ya kuimarisha zaidi Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc),” amesema.

Balozi Mulamula amesema Rais Masasi ataondoka nchini Ijumaa Juni 11, 2021 baada ya kutembelea kituo kimoja wapo cha biashara hapa nchini (ambacho hakukitaja).

 

Leave A Reply