The House of Favourite Newspapers

Rais wa Ukrain Alaani Mashambulio ya Urusi Dhidi ya Nchi Yake

0
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

RAIS wa Ukraine Volodymyr Zelensky amelaani shambulio dhidi ya makazi ya watu katika mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, ambalo alilitaja kuwa la ‘kudharauliwa’.

 

Shambulio hilo limeacha maafa kwa kusababisha vifo vya watu 6 na kuacha majeruhi zaidi ya 16 katika mji wa Kharkiv ambao ni wapili kwa ukubwa.

 

Rais Volodymyr Zelenskyy alisema jengo la ghorofa “limeharibiwa kabisa” katika shambulio la Jumatano usiku, ambalo alisema “shambulio hilo halikuwa na sababu yoyote na inaonyesha kutokuwa na nguvu kwa mvamizi(Urusi)”.

 

Amesema kwamba hawatasamehe kutikana na shambulio hilo na wanajipanga kulipa kisasi kwa Urusi.

 

Timu ya wanahabari ya Zelenskyy ilishiriki picha za matukio ya shambulio hilo, zikionyesha huduma za dharura zikiwa nje ya jengo hilo linalowaka moto.

 

Sauti kwenye video hiyo ilielezea tukio hilo na kusema watu wengi hawakujulikana waliko.

Shambulio katika mji wa Kharkiv limesababisha mauaji ya watu 6 na wengine wengi kujeruhiwa

“Kwa bahati mbaya, idadi ya waliokufa na kujeruhiwa katika shambulio la makombora katika wilaya ya Saltivka imeongezeka hadi sita waliokufa na 16 kujeruhiwa,” Gavana wa mkoa Oleg Synehubov alisema kwenye mtandao Telegram.

 

Kharkiv ilikuwa shabaha ya Urusi katika siku za mwanzo za vita, lakini askari wake hawakuweza kuuteka mji huo.

 

Wakati Moscow sasa imehamishia mwelekeo wake wa kijeshi mashariki na kusini mwa Ukraine, Kharkiv inaendelea kukumbwa na mashambulizi ya angani.

 

Imeandikwa: Dunstan Mtili Erick kwa msaada wa mitandao.

Leave A Reply