RAMMY, JINA LA KANUMBA FEKI LILINIHARIBU KISAIKOLOJIA

Muigizaji mahiri wa kiume wa Bongo Muvi, Rammy Gallis, amesema kuwa hakuna kitu kilichokuwa kikimuharibu kisaikolojia akilia mara kwa mara kama kuitwa Kanumba Feki.

 

Akipasha habari na Za Motomoto, Rammy alisema kuwa mtu alipokuwa akimuita Kanumba Feki alikuwa akiteseka kisaikolojia maana tayari alikuwa akiona watu wanamchukulia hata kuigiza kwake ni feki wakati na yeye msanii na alitaka kutoka kivyake.

 

“Kwa kweli hakuna kitu kilichoniharibu kisaikolojia kama nilivyokuwa nikiitwa Kanumba Feki na sio kwamba nilikuwa simpendi kaka yangu aliyetangulia mbele ya haki bali nilitaka nitoke kivyangu na jina langu libaki tu kufanana kama wanavyosema,” alisema Rammy.

Loading...

Toa comment