The House of Favourite Newspapers

Rapa Future Ategemea Mtoto wa 5 na Joice Chavis

RAPA Mmarekani, Future, jana alihudhuria sherehe ya kumkaribisha kijacho wake wa tano kutoka kwa  Joie Chavis, ambaye pia ni mama-watoto wa rapa Bow Wow.

Mastaa hao walikutana baada ya kufarakana kwa miezi kadhaa na jana walionekana kuwa wenye furaha kubwa katika tukio hilo.

 

Mtoto anayetegemewa, ambaye ni wa kiume,  ataungana na familia kubwa mchanganyiko ambapo mama yake ana binti aliyezaa na rapa Bow Wow, ambapo Future ana mtoto wa kiume aliyezaa na Ciara.

Future atakayekuwa amepata watoto watano aliozaa na wanawake  watano, aliungana na mama-watoto wake wa kwanza,  Brittni Mealy, ambaye alishiriki katika hafla hiyo ya Chavis.

 

Comments are closed.