The House of Favourite Newspapers

Ratiba ya Robo Fainaili Ligi ya Mabingwa Ulaya

0

uefa

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, hivi punde limetoa ratiba ya mechi za Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya ambayo inaingia katika hatua ya robo fainali.

Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA uliopo mjini Nyon nchini Uswizi, kwa kuwashirikisha maofisa wa klabu zote nane ambazo zilifanikiwa kupenya katika hatua ya 16 bora.

Michezo ya hatua ya robo fainali imepangwa kuchezwa Aprili 5 na 6 na marudio ni Aprili 12 na 13.

Ratiba yenyewe ipo kama ifuatavyo:

Barcelona Vs Atletico Madrid

Bayern Munich Vs Benfica

Paris Saint Germain Vs Manchester City

Wolfsburg Vs Real Madrid

Leave A Reply