The House of Favourite Newspapers

RAYVANNY AWASHANGAA WANAOSEMA ANAJICHUBUA

MSANII wa lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Ray­mond Mwakyusa ‘Rayvanny’ amewashangaa wanaomsema vibaya kuwa anajichubua, kitendo ambacho hajawahi kukifikiria katika maisha yake.

 

Akipiga stori na Ijumaa Wikienda, Rayvanny alisema kuwa anashangaa maneno hayo yanatoka wapi kwani katika maisha yake haja­wahi kuwaza kufanya hivyo na anachoamini yeye watu watakuwa wanaongea kwa sababu ya muonekano wake kwenye picha.

 

“Jamani mimi hizo tabia nimezianza lini tena? Yaani walimwengu hawakosagi cha kusema, unajua kuna picha ambazo zikitupiwa mtandao­ni naonekana mweupe sana na nyingine zinakuwa zime­toka vibaya, hapo watu ndiyo huanza kusema nimejichibua, kitu ambacho siyo kweli,” alisema Rayvanny.

 

Hivi karibuni msanii huyo aliposti picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa ana­toka kwenye mahojiano na moja ya vyombo vya habari hapa nchini, ambapo picha hiyo ilionesha magoti yake ni meusi tofauti na sehemu nyingine za mwili wake hivyo kuwafanya wadau kudhani amejichubua.

STORI: Memorise Richard, Ijumaa Wikienda

Watoto Waliowashinda WEMA na GABO Kwenye Tuzo Wafunguka “HATUKUTEGEMEA”

Comments are closed.