The House of Favourite Newspapers

RAYVANNY: MAMA WATOTO AKITEMBEA UTUPU POA TU

Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ na Fayma ‘Fayvanny’

MWANAMUZIKI kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ amefunguka kwamba, kwa dunia ilipofikia sasa kwa upande wake suala la mavazi siyo ishu, hata kama mpenzi wake aliyezaa naye mtoto mmoja akitembea utupu hajali.  Akichonga na Risasi Vibes, Rayvanny alisema suala la muhimu kwa sasa ni uaminifu na mapenzi ya dhati kutoka kwa wapendanao, lakini suala la mavazi ni uchaguzi tu.

“Mtu akiwa mhuni hata avae muda wote dela au ushungi, akiamua kupata wanaume atawapata tu na mavazi kwa sasa hayatafsiri tabia ya mtu, bali ni namna mtu anavyovutiwa kuonekana. “Mimi hata siku moja siwezi kumpangia mpenzi wangu avae kwa namna gani, vyovyote anavyopenda mimi fresh tu hata akisema anataka atoke utupu na kuzunguka mitaani poa tu,” alisema Rayvanny.

Akizungumzia safari yake ya Nigeria. Mkali huyo alisema huko alikwenda kikazi na amefanikiwa kufanya kolabo na wasanii wengi wakiwemo Kiss Daniel na Phyno lakini pia nina kazi ambayo imetengenezwa na muandaaji maarufu wa muziki duniani Swizz Beats.

 

Comments are closed.