The House of Favourite Newspapers

RC Ally Hapi Atembelea Ofisi za Global Group – Pichaz

Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Salum Hapi,  akishuka kwenye gari baada ya kuwasili katika ofisi za Global Group, alipozitembelea leo Agosti 30, 2018.

MKUU wa Mkoa wa Iringa, Ally Salum Hapi,  leo Alhamisi, Agosti 30, 2018 ametembelea ofisi za makampuni ya Global Group zilizopo Sinza-Mori jijini Dar es Salaam kisha kuzungumza na viongozi na wafanyakazi wa makampuni hayo.

Hapi akisalimiana na Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho.  Katikati ni Mkuu wa Global TV Online, James Range.

Ofisi za Global Group zinajumuisha kampuni ya mbalimbali zikiwemo Global Digital na Global Publishers inayochapisha magazeti ya Uwazi, Ijumaa, Risasi, Amani, Ijumaa WikiendaChampioni na Spoti Xtra.

Hapi akisalimiana na Mhariri mwandamizi, Elvan Stambuli.

Kiongozi huyo alipata fursa ya kuelezwa na viongozi wa kampuni na wa vitengo mbalimbali namna ambavyo kampuni hizo zimekuwa zikifanya kazi ikiwa ni pamoja na ukusanyaji na uandaaji wa habari, uandaaji wa gazeti (kusanifu kurasa) na usambazaji magazeti hayo kwenda kwa wasomaji.

…Akisalimiana na Mhariri Kiongozi wa Global Publishers, Amrani Kaima.

Aidha, Hapi ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kabla ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, amepata fursa ya kuzungumza na waandishi na wahariri wa magazeti hayo ya Global Publishers ambayo kwa sasa yanaendesha promosheni kabambe ya Tusua Maisha na Global ambapo washindi wanajipatia zawadi za pikipiki, dinner set, ada za shule za watoto wao na jezi za soka kila wiki.

…Akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Ijumaa Wikienda, Sifael Paul.
…Akisaini katika kitabu cha wageni kwenye chumba cha mapokezi.
…Akionyeshwa makampuni yaliyomo ndani ya Global Group.
Kaima akimwonyesha Hapi magazeti yanayochapishwa na Global Publishers kwa wiki.

…Akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Amani ambalo  huwa mitaani kila Alhamisi, Erick Evarist.

…Akionyeshwa moja ya habari ndani ya gazeti a Amani, toleo la leo, Agosti 30, 2018.
Mkuu wa Idara ya Usambazaji, Gasper Urio, akimpa maelekezo Hapi namna ambavyo wanasambaza magazeti na kuwafikia wasomaji wote kwa wakati.
…Akisalimiana na Mhariri wa Gazeti la Championi Jumatatu, Ezekiel Kitula.
…Akisalimiana na mwandishi wa gazeti la Championi, Khadija Mngwai.
…Akisalimiana na mwandishi wa gazeti la Championi, Ibrahim Mussa.
…Akisalimiana na mpigapicha wa Championi, Musa Mateja.
…Akitazama namna ambavyo gazeti linasanifiwa; anayeandaa gazeti hilo ni msanifu kurasa, Shafii Mlaponi.
…Akiendelea kupata maelekezo.
….Akisalimiana na Mkuu wa Idara ya Usanifu Kurasa, Bahati Haule.
Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya Global Group, Eric Shigongo,  akimkaribisha Hapi ofisini kwake.
Wakibadilishana mawazo.
….Akiwa na viongozi nje ya jengo la ofisi za Global Group.

 

PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.